[go: nahoru, domu]

Nenda kwa yaliyomo

Lugha za Kibantu : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
 
(marekebisho 6 ya kati na watumizi wengine 4 na yule ambaye hajaonyeshwa)
Mstari 2: Mstari 2:
'''Lugha za Kibantu''' ni kundi la [[lugha]] ambalo ni [[tawi]] la [[lugha za Niger-Kongo]].
'''Lugha za Kibantu''' ni kundi la [[lugha]] ambalo ni [[tawi]] la [[lugha za Niger-Kongo]].


Lugha za Kibantu huzungumzwa hasa katika nchi za [[Nigeria]], [[Kamerun]], [[Guinea ya Ikweta]], [[Gabon]], [[Jamhuri ya Kongo]], [[Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo]], [[Rwanda]], [[Burundi]], [[Uganda]], [[Kenya]], [[Tanzania]], [[Komori]], [[Msumbiji]], [[Malawi]], [[Zambia]], [[Zimbabwe]], [[Angola]], [[Namibia]], [[Botswana]], [[Lesotho]], [[Swaziland]] na [[Afrika ya Kusini]].
Lugha za Kibantu huzungumzwa hasa katika nchi za [[Nigeria]], [[Kamerun]], [[Guinea ya Ikweta]], [[Gabon]], [[Jamhuri ya Kongo]], [[Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo]], [[Rwanda]], [[Burundi]], [[Uganda]], [[Kenya]], [[Tanzania]], [[Komori]], [[Msumbiji]], [[Malawi]], [[Zambia]], [[Zimbabwe]], [[Angola]], [[Namibia]], [[Botswana]], [[Lesotho]], [[Eswatini]] na [[Afrika ya Kusini]].


Uenezi huo unaonyesha kwamba kundi la lugha za Kibantu ni kubwa kabisa [[bara]]ni [[Afrika]], na [[idadi]] ya wanaozitumia ni takriban watu [[milioni]] 310.
Uenezi huo unaonyesha kwamba kundi la lugha za Kibantu ni kubwa kabisa [[bara]]ni [[Afrika]], na [[idadi]] ya wanaozitumia ni takriban watu [[milioni]] 310.


[[Neno]] '''Bantu''', maana yake ni ''watu'' katika lugha nyingi za kundi hilo. [[Shina]] lake ni ''-ntu'', na [[kiambishi awali]] cha ''ba-'' kinaonyesha [[uwingi]] wa [[viumbehai]]. Kwa sababu hiyo, [[mtaalamu]] [[Wilhelm Heinrich Immanuel Bleek]] (aliyeishi tangu mwaka [[1827]] hadi [[1875]]) alitumia neno hilo kwa kurejea kundi la lugha hizo. Bleek alilinganisha [[sarufi]] za lugha mbalimbali za Kibantu, na baadaye [[Carl Meinhof]] alimfuata katika [[utafiti]] huo.
[[Neno]] ''Bantu'', maana yake ni ''watu'' katika lugha nyingi za kundi hilo. [[Shina]] lake ni ''-ntu'', na [[kiambishi awali]] cha ''ba-'' kinaonyesha [[uwingi]] wa [[viumbehai]]. Kwa sababu hiyo, [[mtaalamu]] [[Wilhelm Heinrich Immanuel Bleek]] (aliyeishi tangu mwaka [[1827]] hadi [[1875]]) alitumia neno hilo kwa kurejea kundi la lugha hizo. Bleek alilinganisha [[sarufi]] za lugha mbalimbali za Kibantu, na baadaye [[Carl Meinhof]] alimfuata katika [[utafiti]] huo.


Kuna ma[[mia]] ya lugha za Kibantu; [[wataalamu]] wengine wanahesabu 300, wengine wanahesabu 600. Mtaalamu [[Malcolm Guthrie]] aliziainisha kulingana na maeneo ya ki[[jiografia]]. Kila eneo limepata [[herufi]] yake — A, B, C, D, E, F, G, H, K, L, M, N, P, R na S — na ndani ya kila eneo kuna [[tarakimu]] tena. Pia, Guthrie alichunguza [[lugha ya nasaba]] ambayo ni chanzo cha lugha zote za Kibantu.
Kuna ma[[mia]] ya lugha za Kibantu; [[wataalamu]] wengine wanahesabu 300, wengine wanahesabu 600. Mtaalamu [[Malcolm Guthrie]] aliziainisha kulingana na maeneo ya ki[[jiografia]]. Kila eneo limepata [[herufi]] yake — A, B, C, D, E, F, G, H, K, L, M, N, P, R na S — na ndani ya kila eneo kuna [[tarakimu]] tena. Pia, Guthrie alichunguza [[lugha ya nasaba]] ambayo ni chanzo cha lugha zote za Kibantu.
Mstari 21: Mstari 21:


''(Idadi ya wasemaji ni makadirio tu; bado ina tofauti kati ya makala na makala)''
''(Idadi ya wasemaji ni makadirio tu; bado ina tofauti kati ya makala na makala)''
* [[Kiswahili]] na [[lahaja]] zake (wasemaji milioni 150<ref>{{Cite web|title=Swahili|url=https://clp.arizona.edu/swahili|work=Critical Languages Program|date=2016-04-12|accessdate=2020-01-30|language=en}}</ref>) : [[Tanzania]], [[Kenya]], [[Uganda]], [[Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo]], [[Rwanda]], [[Burundi]], [[Komori]], [[Mayotte]], [[Msumbiji]], [[Somalia]].
* [[Kiswahili]] na [[lahaja]] zake (wasemaji milioni 150<ref>{{Cite web|title=Swahili|url=https://clp.arizona.edu/swahili|work=Critical Languages Program|date=2016-04-12|accessdate=2020-01-30|language=en|archiveurl=https://web.archive.org/web/20190504081655/https://clp.arizona.edu/swahili|archivedate=2019-05-04}}</ref>): [[Tanzania]], [[Kenya]], [[Uganda]], [[Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo]], [[Rwanda]], [[Burundi]], [[Komori]], [[Mayotte]], [[Msumbiji]], [[Somalia]].
* [[Kinyarwanda]]-[[Kirundi]] : (wasemaji milioni 15): Rwanda, Burundi
* [[Kinyarwanda]]-[[Kirundi]] : (wasemaji milioni 15): Rwanda, Burundi
* [[Lingala]] (wasemaji milioni 10): [[Angola]], [[Jamhuri ya Afrika ya Kati]], [[Jamhuri ya Kongo]], Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, [[Gabon]]
* [[Lingala]] (wasemaji milioni 10): [[Angola]], [[Jamhuri ya Afrika ya Kati]], [[Jamhuri ya Kongo]], Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, [[Gabon]]
Mstari 32: Mstari 32:
* [[Chiluba]] (wasemaji milioni 6) : Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, [[Angola]]
* [[Chiluba]] (wasemaji milioni 6) : Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, [[Angola]]


==Tanbihi==
{{reflist}}
{{mbegu-lugha}}
{{mbegu-lugha}}

{{DEFAULTSORT:Bantu}}
{{DEFAULTSORT:Bantu}}
[[Jamii:Makundi ya lugha]]
[[Jamii:Makundi ya lugha]]
[[Jamii:Lugha za Afrika]]
[[Jamii:Lugha za Afrika]]
[[Jamii:Lugha za Kibantu]]
[[Jamii:Lugha za Kibantu| ]]

Toleo la sasa la 15:33, 7 Machi 2024

Ramani hii inaonyesha enezi la lugha za Kibantu (rangi ya machungwa) kulingana na lugha nyingine za Niger-Congo (rangi ya manjano).

Lugha za Kibantu ni kundi la lugha ambalo ni tawi la lugha za Niger-Kongo.

Lugha za Kibantu huzungumzwa hasa katika nchi za Nigeria, Kamerun, Guinea ya Ikweta, Gabon, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Tanzania, Komori, Msumbiji, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Angola, Namibia, Botswana, Lesotho, Eswatini na Afrika ya Kusini.

Uenezi huo unaonyesha kwamba kundi la lugha za Kibantu ni kubwa kabisa barani Afrika, na idadi ya wanaozitumia ni takriban watu milioni 310.

Neno Bantu, maana yake ni watu katika lugha nyingi za kundi hilo. Shina lake ni -ntu, na kiambishi awali cha ba- kinaonyesha uwingi wa viumbehai. Kwa sababu hiyo, mtaalamu Wilhelm Heinrich Immanuel Bleek (aliyeishi tangu mwaka 1827 hadi 1875) alitumia neno hilo kwa kurejea kundi la lugha hizo. Bleek alilinganisha sarufi za lugha mbalimbali za Kibantu, na baadaye Carl Meinhof alimfuata katika utafiti huo.

Kuna mamia ya lugha za Kibantu; wataalamu wengine wanahesabu 300, wengine wanahesabu 600. Mtaalamu Malcolm Guthrie aliziainisha kulingana na maeneo ya kijiografia. Kila eneo limepata herufi yake — A, B, C, D, E, F, G, H, K, L, M, N, P, R na S — na ndani ya kila eneo kuna tarakimu tena. Pia, Guthrie alichunguza lugha ya nasaba ambayo ni chanzo cha lugha zote za Kibantu.

Tabia za Kibantu na historia ya lugha

Lugha za Kibantu zina tabia mbalimbali za pamoja. Kati ya tabia hizo kuna viambishi awali na ngeli za nomino.

Kutokana na sifa hizo wataalamu wamekadiria kwamba asili ya lugha za Kibantu ilikuwa katika maeneo ya Kamerun ya Kusini; kutoka huko wasemaji asilia wa Kibantu katika milenia ya pili KK walihamia Kongo hadi Zambia. Waliendelea kuhamahama na kupanuka hadi kufika maeneo yote walipo sasa.

Sehemu kubwa ya maeneo ya wasemaji wa lugha za Kibantu zilikaliwa awali na wasemaji wa lugha za Khoisan. Wataalamu wamekisia kwamba Wabantu walifaulu kuenea kutokana na maarifa yao ya kilimo na hasa matumizi ya chuma katika zana za kilimo na pia silaha.

Lugha za Kibantu zenye wasemaji wengi

Kati ya lugha za Kibantu zinazotumika zaidi kuna Kiswahili na Kilingala. Lugha zenye wasemaji wengi kama lugha ya kwanza ni Kizulu na Kishona.

(Idadi ya wasemaji ni makadirio tu; bado ina tofauti kati ya makala na makala)

Tanbihi

  1. "Swahili". Critical Languages Program (kwa Kiingereza). 2016-04-12. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-05-04. Iliwekwa mnamo 2020-01-30.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lugha za Kibantu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.