[go: nahoru, domu]

Nenda kwa yaliyomo

Papa Leo I : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d [r2.6.1] roboti Badiliko: tr:Papa I. Leo
Mstari 95: Mstari 95:
[[th:สมเด็จพระสันตะปาปาลีโอที่ 1]]
[[th:สมเด็จพระสันตะปาปาลีโอที่ 1]]
[[tl:León I Magno]]
[[tl:León I Magno]]
[[tr:I. Leo (papa)]]
[[tr:Papa I. Leo]]
[[uk:Лев I]]
[[uk:Лев I]]
[[vi:Giáo hoàng Lêô I]]
[[vi:Giáo hoàng Lêô I]]

Pitio la 19:47, 22 Novemba 2010

Papa Leo Mkuu

Papa Leo I (400 hivi – 10 Novemba 461) alikuwa papa kwa muda mrefu, kuanzia 29 Septemba, 440 hadi kifo chake. Jina lake la kuzaliwa pia lilikuwa Leo. Alimfuata Papa Sixtus III.

Alikuwa kwa asili sharifu wa Italia, akawa papa wa kwanza kuitwa "Mkuu" kutokana na mchango wake mkubwa upande wa dini na wa siasa.

Anaheshimiwa kama mtakatifu, babu wa Kanisa na mwalimu wa Kanisa.

Asili na ujana

Alizaliwa katika mkoa wa Toscana (Italia ya kati).

Mwaka 431, akiwa shemasi, pengine aliandikiwa na Cyril wa Aleksandria ili kuungwa mkono dhidi ya Juvenali wa Yerusalemu. Wakati huohuo Yohane Kasiano alimuandikia kitabu dhidi ya Nestori wa Konstantinopoli. Hasa kaisari alimteua kuwapatanisha maofisa wakuu wa Gallia (leo Ufaransa).

Akiwa huko, Papa Sixtus III alifariki (11 Agosti 440), na Leo alichaguliwa na umati kwa kauli moja kushika nafasi yake. Tarehe 29 Septemba Leo alianza kazi yake kama papa ambayo ilichangia sana kukusanyia Roma mamlaka ya Kanisa lote.

Papa

Nafasi bora ya kusisitiza mamlaka hiyo hata upande wa mashariki ilitolewa na mabishano kuhusu nafsi ya Yesu Kristo yaliyosababishwa na Eutike.

Mwaka 451 katika Mtaguso wa Kalsedonia, baada ya barua yake kwa Flavianus kusomwa, maaskofu wote walisimama na kulia: "Ndiyo imani ya mababu... Mtume Petro amesema kwa njia ya Leo..."

Vilevile, Leo alipambana na Wapelaji, Wamani na Waprishila.

Siasa

Mchoro wa Raffaello kuhusu Leo Mkuu kukutana na Atila.

Wakati Dola la Roma lilipokuwa likisambaratika, Leo alipata umaarufu pia kwa kutumia mamlaka yake ya kiroho kuzuia uvamizi wa Roma uliohofiwa kufanywa na Atila, mfalme wa Wauni.

Umuhimu wa Leo

Umuhimu wa upapa wa Leo, ambao ulidumu muda mrefu kuliko mapapa karibu wote, ni katika kusisitiza mamlaka ambayo Kanisa la Roma linayo juu ya makanisa yote duniani kutokana na Mtume Petro. Ndiyo fundisho linalojitokeza katika barua zake na hasa katika hotuba 96 zilizopo hata leo.

Vyanzo

  • Louise Ropes Loomis, The Book of Popes (Liber Pontificalis). Merchantville, NJ: Evolution Publishing. ISBN 1-889758-86-8 (Reprint of the 1916 edition. English translation with scholarly footnotes, and illustrations).
  • T. Jalland, The Life and Times of St. Leo the Great, (London, 1941).

Viungo vya nje