Ankara
Ankara ni mji mkuu wa Uturuki. Iko katika kitovu cha Anatolia kwenye kimo cha 938 m juu ya UB.[1] Huu ndiyo mji mkuu wa Mkoa wa Ankara.
Jiji la Ankara | |
Mahali pa mji wa Ankara katika Uturuki |
|
Majiranukta: 39°52′N 32°52′E / 39.867°N 32.867°E | |
Nchi | Uturuki |
---|---|
Tovuti: www.ankara.bel.tr./ |
Ankara ni mji mkubwa wa pili nchini baada ya Istanbul. Kuna wakazi 4,319,167 (2005).
Historia
Ankara ilianzishwa katika milenia ya pili KK na tangu karne ya tatu KK ilijulikana kwa jina la Ancyra. Wakatai wa Dola la Roma ilikuwa mji mkuu wa jimbo la Galatia. Mji uliendelea katika Dola la Bizanti (Roma ya Masahriki).
Tangu mwaka 1071 makabila ya Waturuki walianza kuvamia Anatolia na Sultani Alparslan alitwaa mji mwaka 1073 ukawa sehemu ya falme mbalimbali ya kituruki hadi kuja kwa Dola la Uturuki wa Waosmani.
Baada ya kushindwa kwa Uturuki katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia nchi washindi hasa Uingereza, Ufaransa, Italia na Ugiriki zilianza kugawa mabaki ya Dola la Uturuki. Kiongozi wa upinzani wa kitaifa wa Kituruki jenerali Kemal Atatürk alichagua Ankara kama makao makuu ya upinzani mwaka 1919.
Baada ya vita ya uhuru wa Uturuki mwaka 1923 nchi ilitangazwa kuwa jamhuri na Ankara mji wake mkuu badala ya Istanbul iliyowahi kuwa mji wa masultani.