[go: nahoru, domu]

Almas Tower (Kiarabu:برج الماس) Diamond Tower) ni jumba refu sana mjini Dubai, United Arab Emirates. Ujenzi wa jengo hili la ofisi ilianza mapema mwaka 2005 na kukamilika mwaka 2009. Jengo hili lilifika urefu wake kamili mwaka 2008, na kuwa jengo ja pili refu zaidi Dubai, baada ya Burj Khalifa. Jumba hili lina ghorofa 74, 70 ambazo ni za kutumika kwa biashara sambamba na ghorofa nne za huduma.

Almas Tower
Ujumbe wa Ujumla
HaliCompleted


Jumba hili liko kwenye kisiwa bandia chake mwenyewe katikati mwa mfuko wa Jumeirah Lake Towers, jumba hili ndilo refu zaidi katika majumba yote yatakayojengwa katika mfuko huo baada ya ujenzi kukamilika. Ilibuniwa na kampuni ya Atkins Middle East, ambao walibuni asilimia kubwa ya jumba la JLT. Jumba hili linajengwa na Taisei Corporation ya Japan katika ubia na ACC (Arabian Construction Co) ambao walishinda mkataba wa Nakheel tarehe 16 Julai 2005. [1]


Kampuni ya Dubai Multi Commodities Centre (DMCC), wamiliki wa jumba, walikuwa wa kwanza kuhamia. DMCC walihamisha ofisi zao pamoja na Dubai Diamond Exchange kabla jumba hili likamilike tarehe 15 Novemba 2008. [2] Almas Tower sasa ina manyumba ya kutoa huduma za aina nyingi za almasi ya kanda ile, vito vya thamani na viwanda vwa lulu. Pamoja na Dubai Diamond Exchange, hizi ni pamoja na Dubai Diamond Exchange, Dubai Pearl Exchange, Dubai Gems Club, Kimberley Process, ofisi za kupate vyeti na upatikanaji wa huduma bora za usafirishaji kutoka makampuni kama Brinks na Transguard. Kukatwa kwa Almasi na kubadilishana hufanyiwa huko ndani. Kutokana na aina ya mashirikiano yanayofanyika kwenye jumba hili, kuna usalama wa hali ya juu.


Hifadhi ya Picha za Ujenzi


Marejeo


Viungo vya nje

WikiMedia Commons 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:



Kigezo:Dubai skyscrapers Kigezo:Supertall skyscrapers 25°04′08.25″N 55°08′28.34″E / 25.0689583°N 55.1412056°E / 25.0689583; 55.1412056