[go: nahoru, domu]

Havana

Pitio kulingana na tarehe 14:26, 22 Aprili 2015 na Dexbot (majadiliano | michango) (Removing Link FA template (handled by wikidata))


Havana (kihisp. La Habana) ni mji mkuu na mji mubwa wa Kuba kwenye 23°8′N 82°23′W. Kuna wakazi milioni 2.2. Tangu 1982 mji wa kale umepokelewa katika orodha ya urithi wa dunia.

Jiji la Havana
Nchi Kuba
Faili:LaHabana.jpg
Havana wakati wa jioni
Mahali pa Havana nchini Kuba

Historia

Mji kwa jina la Havana ulianzishwa 1515 na Mhispania Diego Velázquez de Cuéllar lakini ulihamishwa mwaka 1519 kuja mahali pa kudumu uliopo hadi leo. Mji ukakua kuwa bandari muhimu wa kijeshi na kibiashara. Tangu 1607 Havana ilikuwa mji mkuu wa koloni ya Kihispania ya Kuba.

Havana ilikuwa hasa tangu azimio la Hispania la kukusanya "la flota" yaani jahazi za kubebea fedha na bidhaa za Amerika kama kundi kabla ya kuvuka Atlantiki kwa kusudi la kuzuia maharamia Waingereza waliovinda meli za Hispania. Azimio hili lilisababisha mamia ya jahazi kukusanyika katika hori ya bahari mbele ya Havana katika miezi ya Mei hadi Agosti mpaka kuanza safari ya pamoja.

Katika karne za 17 na 18 mji uliendelea kukua kuwa mji mkubwa wa tatu wa Amerika baada ya Mji wa Mexiko na Lima kushinda Boston na New York.

Mwisho wa karne ya 19 Havana iliona mlipuko wa manowari SS Maine katika bandari yake tarehe 15 Februari 1898 ulioanzisha vita ya Marekani dhidi Hispania. Havana ilivamiwa na Waamerika na kutangazwa kuwa mji mkuu wa Jamhuri ya Kuba mwaka 1902.

Athira ya Amerika iliendelea kuwa kubwa hadi mapinduzi ya Kuba na kuingia kwa jeshi la mapinduzi chini ya Fidel Castro tarehe 1 Januari 1959.