[go: nahoru, domu]

Ipagala

Pitio kulingana na tarehe 14:06, 25 Septemba 2015 na Dexbot (majadiliano | michango) (Bot: Parsoid bug phab:T107675)

Huwezi kutamka neno Ipagala bila kugusia KKKT IPAGALA hili ni Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania lililo umbali wa km nne tu toka katikati ya Jiji la Kisiasa la Tanzania. Pamoja na Ibada na Mambo mengi yanayoendelea katika Usharika huu tumekuwa Baraka tumekuwa Baraka sana katika Eneo hili Ukifika Dodoma Tafadhali usisite kututembelea. Soma Historia yetu kwa ufupi hapo chini.

1.0 Utangulizi:

Usharika wa Ipagala unaongozwa na Mchungaji Menard Simon Kipyali. Mchungaji anasaidiwa na Parish Worker Aichiwailia Malisa. Pia tunao watumishi wengine walioajiriwa na Usharika kwa ajili ya huduma mbalimbali kama vile kufundisha Muziki, kazi ya Ulinzi, Uhasibu na huduma za Usafi katika maeneo yote yanayolizunguka Kanisa. Aidha mambo ya Utawala ya siku kwa siku yanaongozwa na timu ya Utawala yenye watu wanne, yaani Mchungaji,Katibu wa Usharika ,Katibu Msaidizi na Mtunza Hazina wa Usharika.

== 2.0 Historia fupi ya Usharika. Usharika wa Ipagala ulianza kama Mtaa wa Usharika wa Kanisa Kuu Dodoma Mjini tarehe 30/08/2008 Jengo la Ibada lilikuwepo na lilianza kujengwa tarehe 13/9/2006 na ninaposoma taarifa hii Jengo hili bado halijakamilika hivyo bado halijazinduliwa. Mtaa ulianza na Waumini watu wazima 88 na kwa sasa tumeshafikia waumini watu wazima waliojiandikisha 500 na watoto zaidi ya 150. Mwanzoni tulianza na Ibada moja lakini kutokana na ongezeko la waumini tumeongeza Ibada na zimekuwa mbili. Ibada ya kwanza inaanza saa moja na Ibada ya pili inaanza saa nne. Ibada za watoto huenda sambamba na ibada za watu wazima. ==

Usharika wetu uliongozwa na Wachungaji kadhaa kama ifuatavyo:

=== == Jina la Mchungaji Tangu tarehe Hadi tarehe

=

== Mch. Reinhard Riemer 30/08/2008 31/05/2009 ==

== Mch. Joseph Shakato 30/10/2008 21/06/2009 ==

== Mch. Olinde Kataraia 27/09/2009 05/06/2012 ==

== Mch. Menard Kipyali. 06/06/2012 anaendelea ==

Kanisa hili lilianza kujengwa na waumini wa Kanisa Kuu lilipokuwa mtaa na sasa waumini wote wa kanisa hili wanaendelea na Ujenzi kwa kasi nzuri huku Mungu akitusimamia.

== 3.0 Watumishi. 3.1 Walioajiriwa na Dayosisi ==

== Mtumishi aliyeajiriwa na Dayosisi ni mmoja nae ni Mchungaji Menard Simon Kipyali. ==

=== 3.2 Watumishi walioajiriwa na Usharika.

=

== 1. Ndugu Aichiwailia Elimeri Malisa.- ……….Parish worker ==

== 2. Ndugu Jonh Clement Ngaa…………………..Mlinzi ==

== 3. Ndugu Charles Lucas Ngoda…………………Mwanamuziki ==

== 4. Ndugu Elisante Christopher Machange……….Mhasibu ==

== 5. Ndugu Grace Martin Mwinga…………………Mlinzi ==

== 6. Ndugu Paschal William Benedicto…………….Mlinzi ==

== 7. Ndugu Olipa Robert Baharia…………………..Mhudumu

8. Ndugu Apasia Gerald Emmanuel Kileo……….Mhudumu.

== 4.0 Baraza la Wazee. ==

== 1. Mchungaji Menard Kipyali ……….Mwenyekiti ==

== 2. Mzee Mwambene W J……………..Katibu wa Baraza. ==

== 3. Mzee Elisa Maro……………………Mtunza Hazina ==

== 4. Mzee Mary Tarimo…………………Katibu Msaidizi ==

== 5. Mzee Neema Kileo…………………Mwenyekiti Kamati ya Uinjilisti ==

== 6. Mzee Rhoda Bendera………………Mwenyekiti Kamati ya Diakonia ==

== 7. Mzee Annael Malya,……………….Mwenyekiti Kamati ya Malezi ==

== 8. Mzee Laurent Kamayugi…………...Mwenyekiti Uwakili na Miradi ==

== 9. Mzee Grace Tweve………………...Mwenyekiti Kamati ya Fedha ==

== 10. P/ W Aichiwailia Malisa…………...Mjumbe ==

== 11. Mzee Raphael Maro…………………Mjumbe ==

== 12. Mzee Lawrence Lema……………….Mjumbe ==

== 13. Mzee Joshua Msemwa………………Mjumbe ==

== 14. Mzee Atupokile Mwalukasa………....Mjumbe ==

== 15. Mzee Margareth Mkilanya…………..Mjumbe ==

== 16. Mzee Remen Mushi…………………Mjumbe ==

== 17. Mzee Margareth Senkondo…………Mjumbe ==

== 18. Mzee Stanford Mwasumbi………….Mjumbe ==

== 19. Mzee Elihuruma Simon……………..Mjumbe ==

== 20. Mzee Ester Ambakisye………………Mjumbe ==

== 21. Mzee Godfrey Mrutu………………..Mjumbe ==

== 22. Mzee Livingstone Mmari……………Mjumbe ==

== 23. Mzee Lena Mtivike…………………..Mjumbe ==

== 24. Mzee Elizabeth Mgata……………….Mjumbe ==

== 25. Mzee Juliana Mbaga…………………Mjumbe ==

== 26. Mzee Haika Meta……………………Mjumbe ==

== 27. Mzee Tecla Mushi…………………..Mjumbe ==

== 28. Mzee Gibson Sam…………………...Mjumbe ==

== 29. Mzee Justin Thomas…………………Mjumbe ==

== 30. Mzee Mastidia Kashamba……………Mjumbe ==

== 31. Mzee Erick Kitaly……………………Mjumbe ==

== 32. Mzee Rogathe Swai………………….Mjumbe ==

== 33. Mzee Ester Swai…………………….Mjumbe ==

== 34. Mzee Godwin Shembilu…………….Mjumbe ==

== 35. Mzee Joseph Karani…………………Mjumbe ==

== 36. Mzee Semwanga Mwanga…………..Mjumbe ==

== 37. Mzee Merina Temba………………..Mjumbe ==

== 38. Mzee Lucy Sovela…………………..Mjumbe ==

== 39. Mzee Mary Shayo…………………..Mjumbe ==

== 40. Mzee Rehema Kweka………………Mjumbe ==

== 41. Mzee Violet Mwambenja……………Mjumbe ==

42. Mzee Joyce Kafanabo………………Mjumbe

Wazee wote hawa wapo katika Kamati mbalimbali, na Wenyeviti wa Kamati huunda Kamati ya Utendaji. Aidha Baraza la Wazee limeunda Kamati Tatu maalum ambazo hazipo Kikatiba kwa ajili ya kuboresha utendaji katika Usharika wetu.

Kamati hizo ni:

  • Kamati ya Ulinzi na Usalama
  • Kamati ya Mahusiano
  • Kamati ya Ujenzi.

=== == 5.0 Washarika:

=

Tunamshukuru Mungu kwamba Usharika wetu unaendelea kukua kwa kimaendeleo ya Kiroho na Kiuchumi pia. Washarika waliojiandikisha ni 505 na wastani wa mahudhurio kila Jumapili ni 480.

6.0 Huduma za Kiroho.

=== == 6.1 Ibada

=

== Tunayo kila sababu ya kumshukuru Mungu kwani anatuwezesha wakati wote kuwa na Ibada zenye utulivu na uchaji wa nguvu ya Roho mtakatifu. Ibada za kila Jumapili na zile maalum zinafanyika kwa kufuata Kalenda yetu ya KKKT isipokuwa wakati wa Matukio Maalum kama vile Mavuno, Mikutano ya Kiroho n.k. ==

== Ratiba nyingine za Ibada ni kama ifuatavyo: ==

  • Fellowship na Bible study ni kila siku ya Jumatano na Jumapili jioni
  • Ibada za asubuhi ni kila siku kuanzia saa 12:00 hadi saa 12.30. isipokuwa Jumamosi na Jumapili.
  • Ibada za Nyumba kwa Nyumba, hufanyika kila wiki mara moja katika maeneo yetu, tunazo Jumuiya 17. Changamoto kwenye Jumuiya zetu ni mahudhurio hafifu hasa kwa akina Baba. Niwaombe sasa akibaba wote tuanze kuhudhuria kwa wingi kwenye Ibada hizi. Sadaka za Jumuiya huwekwa Benki kwenye account ya Jumuiya.

== 6.2. Sakramenti ya meza ya Bwana. ==

Hufanyika mara moja kila mwezi, Hapa Usharikani na kwa wagonjwa walioko majumbani. Pamoja na hayo huduma hii hutolewa kwa dharura pale inapohitajika.

== 6.3. Kurudi kundini. ==

Huduma hii hutunzwa na Mchungaji Kiongozi ataifafanua vizuri kwenye taarifa ya Kichungaji.

== 6.4. Ndoa. ==

Mchungaji hutunza huduma hii kama ilivyo Sheria, matangazo ya ndoa hutolewa mara tatu ndani siku 21 kabla ya ndoa kufungwa. Kuanzia mwaka 2010 Usharika ulianzisha utaratibu wa kuandaa na kugharamia ndoa za pamoja, ili kutoa fursa kwa Washarika ambao wanapenda kutengeneza mambo yao kwa utaratibu huu. Mwaka huu tunategemea tutaendelea na zoezi hili.

=== ==
6.5. Ubatizo

=

Watu wazina na Watoto hubatizwa kila mara huduma hii inapohitajika, Huduma hii husimamiwa na Mchungaji.

=== == 6.6. Vifo.

=

Usharika hutoa huduma nzuri ya Faraja kwa Familia ya ndugu anaetwaliwa. Ibada ya mazishi huendeshwa kwa utaratibu wa Kanisa na kutunza kumbukumbu zote.

== 6.7. Usuruhishi. ==

Ofisi ya Mchungaji hupokea na kusuluhisha kwa siri kesi zote za kifamilia, ndugu na ndugu, kesi za ndoa, kesi za vikundi n.k. Mara chache sana hushirikisha kamati ya Utawala. Tatizo linapokuwa kubwa hupelekwa Jimboni kwa hatua zaidi.

== 6.8. Huduma za Yatima na misaada mbalimbali. ==

Usharika unatoa misaada mbalimbali kwa Watoto Yatima ikiwa ni pamoja na kulipa karo za shule na mahitaji madogomadogo.

=== == 6.9. Huduma kwa Wajane na Wasiojiweza.

=

Usharika hutoa huduma kwa Wajane na wasiojiweza kwa kuitumia Kamati yetu ya Diakonia. Huduma hizi ni pamoja na za kiroho, za kiuchumi na za kiafya.

== 7.0 Semina Mikutano na Vikao.

==

== 7.1 Semina. ==

Kila mwaka semina mbalimbali zinaendeshwa na Usharika ili kutoa Elimu zaidi ya Kiroho,kijamii, kisheria, kiuchumi n.k. Semina hizi hutolewa kwa ajili ya vikundi vya kwaya wanandoa, akinamama, vijana na wazee wa Baraza. Walimu wa Shule ya Jumapili huandaliwa semina mahususi kwa ajili yao zingine huandaliwa na Jimbo na Dayosisi.

=== == 7.2. Mikutano

=

Kila mwaka tunafanya mikutano ya Injili angalau mara nne na Wahubiri hutoka nje ya Kanisa letu. Mikutano hii imekuwa Baraka kubwa sana kwetu.

== 7.2 Vikao. ==

Vikao vya Kamati Utendaji hufanyika mara moja kila mwezi na kunapokuwa na tukio maalum tunakuwa na vikao vya dharura. Kila robo ya mwaka tunakuwa na kikao cha Baraza la Wazee ambao husomewa taarifa ya fedha ambayo husomwa pia usharikani na washarika hupewa muda wa kuuliza na kupata ufafanuzi pale ambapo hapajaeleweka.

Mala moja kwa mwaka huwa tunakuwa na kikao maalum cha Usharika ambacho Mchungaji hutoa taarifa za Kichungaji. Na hapa huwa tunatoa fursa kwa washarika kuelewa kwa undani zaidi mambo mengi ya kiroho ayafanyayo Mchungaji, pia tunatoa fursa ya maswali ambayo hufanyiwa kazi na Kamati ya Utendaji na Baraza la wazee. Kwa mwaka huu tunatoa taarifa ya Katibu wa Usharika pia.

Tunamshukuru Mungu kwani vikao na mikutano yote hufanyika kwa utulivu na Amani, hali ambayo hupelekea kuweza kupanga na kuamua mambo mengi yanayoleta maendeleo ya Usharika wetu.

8.0.Elimu ya Kikristo

== 8.1.Shule ya Jumapili. ==

== Tunavyo vituo vitatu vinavyotoa elimu ya Kikristo kwa watoto wa shule ya Jumapili ambavyo ni: i).Hapa Usharikani. ii)Jengo la Diakonic centre lililoko Jumuiya ya Kana. iii)Jumuiya ya Yafa. ==

Tunao walimu wa kujitolea 14 katika kila ibada. Pia anakuwepo Mzee mmoja wa Baraza ambae anasali na watoto lakini muhimu zaidi anafuatilia mafunzo yanayotolewa kwa watoto kwa kutambua kuwa watoto ni mhimili mkubwa wa Kanisa.

== 8.2.Elimu ya kikristo mashuleni. ==

== Usharika unatoa Elimu ya kikristo kwa Shule nane kama ifuatavyo: ==

  • Shule ya msingi Ipagala
  • Shule ya msingi Ipagala B
  • Shule ya msingi Chaduru
  • Shule ya msingi makole.
  • Shule ya msingi DCT.
  • Shule ya sekondari Kisasa
  • Shule ya sekondari Doreta
  • Shule ya sekondari Makole.
  • Changamoto kubwa ni kwamba hatuna waalimu kabisa. Ni kazi kubwa kwa Mchungaji wetu kuzungukia shule zote hizi peke yake. Tunaomba wenye uwezo wa kufundisha kwa kujitolea waje tuwape mwongozo wa kuongoza Ibada hizi.

== 8.3. Kipaimara na Nikodemo ==

== Usharika hutoa mafunzo ya miaka miwili kwa wanafunzi wa kipaimara kama ilivyoagizwa na Dayosisi. Pia hutoa mafunzo ya Kipaimara kwa watu wazima- Darasa la Nikodemo. Watumishi wa Usharika hushirikiana katika kufundisha madarasa haya. Na mkuu wa madarasa haya ni Mchungaji. ==

=== == 9.0. Uchumi

=

Uchumi wa Usharika unatokana na sadaka za washarika. Sadaka hizi zimegawanyika katika mafungu yafuatayo:-

  • Ahadi
  • Shukrani
  • Fungu la kumi
  • Sadaka maalum ya Ujenzi.

Mwaka uliopita 2014, Usharika uliweza kukopa sh 55milioni. Kutoka Uchumi Benki iliyoko Moshi, kwa ajili ya ununuzi wa kiwanja cha kujenga Nyumba ya Mtumishi. Tunamshukuru sana Mungu kwani tulikopa deni hili mwezi wa July 2014 na tumelipa deni lote mwezi wa Disemba 2014. kwetu huu ni muujiza.

== 9.1. Miradi. ==

Tunatamani kuwa miradi mbalimbali katika Usharika wetu lakini mpaka sasa hatuna mradi wowote, hii ni changamoto. Mkumbuke wazo la kujenga zahanati na kituo cha watoto katika eneo hili halijafutika, tunatamani kupata mpango kazi wa kuwezesha wazo hili. Naomba nilitoe kwenu kama changamoto.

=== == 10.0. Mahusiano

=

Usharika wetu umeendelea kuwa na mahusiano mazuri ndani ya Jimbo, ndani ya Dayosisi, ndani na nje ya Nchi. Kwa upande wa mahusiano ya nje ya nchi tunaendelea na mahusiano mazuri na ndugu zetu wa Ohio St Martin kule Marekani.

=== == 10.1. Mitaa

=

Usharika wetu hauna Mtaa hata mmoja tunaoutunza.

== 10.2. Vikundi vya Usharika. ==

== Vikundi vya Usharika vinavyotambulika katika taratibu za Usharika wetu. ==

== ni kama ifuatavyo:- ==

== Shule ya Jumapili ==

== Fellowship ==

== Umoja wa Akina Mama ==

== Umoja wa Akin Baba ==

== Umoja wa Vijana ==

== Kwaya ya Usharika ==

== Kwaya ya Ebeneza. ==

Kwaya ya Uinjilisti.

==
11.0. Mipango ya maendeleo ya Usharika kiroho na kiuchumi. ==

11.1. Mipango ya muda mfupi.

  • 1) Kuenelea kuhubiri injili ya kristo na kufundisha neno la Mungu kwa njia zote zinazokubalika Kikristo kwa kufuata taratibu za Kilutheri.
  • 2) Kuendelea kufanya mikutano ya Injili ya nje hapa Usharikani
  • 3) Kuwa na Semina mbalimbali.
  • 4) Kuendelea kununua Samani za Usharika.
  • 5) Kushiriki kikamilifu shughuli mbalimbali za Kijimbo na Dayosisi yetu ya Dodoma.
  • 6) Kuimarisha uhusiano uliopo kati ya ngazi zote.
  • 7) Kuendelea na Ujenzi wa Jengo la Kanisa na Ujenzi wa nyumba ya Mchungaji - tungependa sana Ujenzi uanze mwaka huu.
  • 8) Kuendelea kuimarisha vikundi vya Usharika.
  • 9) Kuhudumia wahitaji kadri Bwana atakavyotujalia.

=== == 11.2. Mipango ya Muda Mrefu.

=

  • I. Ujenzi wa Zahanati
  • II. Ujenzi wa Shule ya awali.
  • III. Kuwa na Hostel
  • IV. Mashine ya kukamua mafuta yatokanayo na nafaka.
  • V. Mashine ya kusaga na kukoboa nafaka.
  • VI. Duka la vitabu
  • VII. Kisima kirefu cha maji.
  • VIII. Shamba kubwa kwa ajili ya mifugo na kilimo.

12.0. Shukrani

Tunamshukuru Mungu wetu tunaemtumikia na kumwabudu sana kwa maana ametenda mambo makuu katika Usharika wetu. Tumeshuhudia uwepo wa Mungu katika kila jambo tunalolifanya kwa utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo. Mafanikio ya kukua kwa Usharika ni kutokana na busara ya viongozi wetu wa Dayosisi, Jimbo, Wachungaji na sisi Washarika wote.

Bwana Yesu Asifiwe!!

Mimi ni

=== == Mzee Mwambene W J

=

Katibu wa Usharika.

==

==

== Kwa niaba ya ==

== Mchungaji Kiongozi Menard Kipyali =

Na Baraza la wazee.