Moses Kulola : Tofauti kati ya masahihisho
Content deleted Content added
Rescuing 2 sources and tagging 0 as dead.) #IABot (v2.0.8 |
|||
(marekebisho 10 ya kati na watumizi wengine 6 na yule ambaye hajaonyeshwa) | |||
Mstari 1:
'''Moses Kulola''' (
==
Pia historia hii inapatikana katika Blog ya [http://tanzaniagospel.blogspot.com/ Tanzania Gospel Network] {{Wayback|url=http://tanzaniagospel.blogspot.com/ |date=20130517045044 }}
Moses Kulola alizaliwa mwezi Juni 1928 katika [[familia]] ya watoto kumi, watano kati yao wakiwa bado hai mwaka 2013.
Alisajiliwa kwanza katika [[shule]] ya [[misheni]] iitwayo Ligsha Sukuma mwaka 1939, halafu alijiunga na [[taasisi]] ya [[usanifu]] mwaka [[1949]].
[[Ubatizo|Alibatizwa]] mwaka [[1950]] katika [[Kanisa la AIC]] Makongoro.
Alimwoa Elizabeth na kuzaliana naye watoto 10 ambapo saba walikuwa bado hai alipofariki.
Alianza kazi za [[umisionari]] mwaka 1950 mara tu baada ya kubatizwa, ijapokuwa aliitwa mwaka 1949.
Mwaka [[1959]] alianza kufanya [[kazi]] [[serikali]]ni, wakati huohuo akihubiri [[Injili]] katika miji na vijiji.
Utumishi wake mkubwa kwa nchi ulifikia mwisho mwaka [[1962]], ambapo aliamua kujitolea moja kwa moja [[nguvu]] zake, [[mwili]] na [[nafsi]].
Mwaka [[1964]] alijiunga na chuo cha [[teolojia]] na [[1966]] alitunukiwa [[stashahada]].
Alijiendelea na masomo mbalimbali ambapo alitunukiwa vyeti katika mataifa mbalimbali.
Alihudumu kikazi kwa miaka miwili kama [[Mchungaji]] kabla ya kuwa [[Mpentekoste]] mnamo [[1961]]-[[1962]].
Alifanya kazi katika [[kanisa la TAG]] tangu mwaka [[1966]] mpaka [[1991]] ambapo aliamua kuanzisha [[kanisa la Evangelistic Assemblies God]] (EAGT), ambalo lilifanikiwa kukua kwa kasi kubwa katika nchi za Tanzania, [[Zambia]], [[Malawi]] na kwa jumla lina makanisa yapatayo 4000 yakiwemo makubwa na madogo.
[[Askofu Msaidizi]] wake alikuwa Mwaisabila.
Kumefanyika mgawanyiko wa ma[[jimbo]] 34 ya kazi na kanda tano kwa ajili ya kurahisisha kazi, kila kanda na jimbo likiwa na mwangalizi wake.
Alifariki mwano Agosti 2013 na kuzikwa mjini [[Mwanza]] katika kanisa linalogombaniwa na TAG na EAGT.
==Viungo vya nje==
* '''''(en)''''' [http://tanzaniagospel.blogspot.com/2012/07/history-of-bishop-kulola-historia-ya.html Askofu Kulola asimulia maisha yake kwenye blogu ya Tanzania Gospel] {{Wayback|url=http://tanzaniagospel.blogspot.com/2012/07/history-of-bishop-kulola-historia-ya.html |date=20160305125254 }}
==Tanbihi==
<references/>
{{DEFAULTSORT:Kulola, Moses}}
[[Jamii:
[[Jamii:Waliozaliwa 1928]]
[[Jamii:Waliofariki 2013]]
|