[go: nahoru, domu]

Moses Kulola (Juni 1928 - Agosti 2013) alikuwa ni kiongozi wa Kikristo nchini Tanzania na tangu 1991 askofu wa EAGT (Evangelistic Assemblies of God Tanzania).

Wasifu

Kulola alizaliwa mwezi Juni 1928 katika familia ya watoto kumi na kufariki mwezi Agosti 2013 katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam. Alisomea shule ya msingi ya Ligsha Sukuma, halafu taasisi ya usanifu. Alibatizwa kikristo mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro. Alimwoa Elizabeth wakawa na watoto kumi.

Alifanya kazi ya uchungaji wa kanisa la AIC miaka ya 1961-1962 akaendelea na masomo ya kitheolojia. Baada ya kujiunga na dhehebu la kipentekoste alifanya kazi ya uchungaji ndani ya kanisa la TAG miaka ya 1966-1991. Akajitenga na kanisa hilo na kuanzisha kanisa jipya mwaka wa 1991, kanisa la EAGT (kwa Kiingereza Evangelistic Assemblies of God) akawa askofu wao wa kwanza tangu mwaka uleule.

Viungo vya nje