[go: nahoru, domu]

Moses Kulola (Juni 1928 - Agosti 2013) alikuwa ni kiongozi wa Kikristo nchini Tanzania na tangu 1991 askofu wa EAGT (Evangelistic Assemblies of God Tanzania).

[1] Moses Kulola, alizaliwa mwezi Juni 1928, katika familia ya watoto kumi, na watano kati yao bado ni hai. nilisajiliwa katika shule yangu ya kwanza mwaka 1939 iitwayo Ligsha Sukuma shule ya misheni baada ya Ligsha, nilijiunga na taasisi ya usanifu mwaka 1949. Nilibatizwa mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro.

Nilimwoa Elizabeth na nina watoto10 ambapo saba bado hai.Nilianza kazi za kimisionari mwaka1950 japokuwa niliitwa mwaka 1949 mara tu baada ya kubatizwa.

Mwaka 1959 nilianza kufanya kazi serikalini, wakati huo huo nikihubiri Injili katika miji na vijiji. Utumishi wangu mkubwa kwa nchi ulifika mwisho mwaka 1962, ambapo niliamua kujitolea moja kwa moja nguvu zangu, mwili na nafsi. Mwaka 1964 nilijiunga na chuo cha kiteolojia na 1966 nilitunukiwa stashahada.

Sikuacha elimu pale tu, nilijiendelea na masomo mbalimbali ambapo nilitunukiwa vyeti mbalimbali katika mataifa mbalimbali.

Nilihudumu kikazi kwa miaka miwili kama Mchungaji kabla ya kuwa mpentekoste mnamo 1961-1962, nilifanya kazi katika kanisa la TAG 1966 mpaka 1991 ambapo nikaamua kuanzishaa makanisa Evangelistic Assemblies God (EAGT), ambapo yalifanikiwa kukua kwa kasi kubwa katika nchi za Tanzania, Zambia , Malawi na kwa ujumla tuna makanisa yapatayo 4000 katika jinsi mbalimbali yakiwemo makubwa na madogo.

Askofu Moses Kulola anayeongoza makanisa elfu nne, Askofu Msaidizi wake ni Mwaisabila.

Mchakato wa kuongoza makanisa elfu nne si rahisi na kwamba kumefanyika mgawanyiko wa majimbo 34 ya kazi na kanda tano kwa ajili ya kurahisisha kazi na kila kanda na jimbo lina mwangalizi wake.

--majadiliano (majadiliano) 21:44, 6 Novemba 2013 (UTC) (maelezo na picha http://sayuni.blogspot.com , imetafsiriwa na tanzaniagospel.blogspot.com)

Viungo vya nje

  1. tanzaniagospel.blogspot.com