Jimbo Katoliki la Wote
Mandhari
Jimbo Katoliki la Wote ni mojawapo kati ya majimbo 27 ya Kanisa Katoliki nchini Kenya. Limeanzishwa tarehe 22 Julai 2023 kwa kumegwa kutoka Jimbo Katoliki la Machakos.
Liko chini ya jimbo kuu la Nairobi.
Lilianzishwa likiwa na eneo la km2 8,009, Wakatoliki 388,946 kati ya wakazi 987,653, parokia 31, mapadri 90 wanajimbo na 9 wamisionari, mashemasi 3, waseminari 36 na makatekista 732.
Askofu wa kwanza ni Paul Kariuki Njiru, akiwa na makao makuu mjini Wote.
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Wote kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |