[go: nahoru, domu]

Nenda kwa yaliyomo

Lugha za Kibantu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 09:56, 20 Januari 2012 na WikitanvirBot (majadiliano | michango) (r2.7.1) (roboti Badiliko: az:Bantu dilləri)
Ramani hii inaonyesha enezi la lugha za Kibantu (rangi ya machungwa) kulingana na lugha nyingine za Niger-Congo (rangi ya manjano).

Lugha za Kibantu ni kundi la lugha ambalo ni tawi la lugha za Niger-Kongo.

Lugha za Kibantu huzungumzwa hasa katika nchi za Kamerun, Nigeria, Gabon, Guinea ya Ikweta, Kongo zote mbili, Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Tanzania, Angola, Zambia, Malawi, Msumbiji, Zimbabwe, Namibia, Botswana, Lesotho, Swaziland na Afrika ya Kusini.

Enezi hilo linaonyesha kwamba kundi la lugha za Kibantu ni kubwa kabisa barani Afrika, na idadi ya wanaozitumia ni takriban milioni 310.

Neno Bantu, maana yake ni watu katika lugha nyingi za kundi hilo. Shina lake ni -ntu, na kiambishi awali cha ba- kinaonyesha uwingi. Kwa sababu hiyo, mtaalamu Wilhelm Heinrich Immanuel Bleek (aliyeishi 1827 hadi 1875) alitumia neno hilo kwa kurejea kundi la lugha hizo. Bleek alilinganisha sarufi za lugha mbalimbali za Kibantu, na baadaye Carl Meinhof alimfuata katika utafiti huo.

Kuna mamia ya lugha za Kibantu; wataalamu wengine wanahesabu 300, wengine wanahesabu 600. Mtaalamu Malcolm Guthrie aliziainisha kulingana na maeneo ya kijiografia. Kila eneo limepata herufi yake—A, B, C, D, E, F, G, H, K, L, M, N, P, R na S—na ndani ya kila eneo kuna tarakimu tena. Pia, Guthrie alichunguza lugha ya nasaba ambayo ni chanzo cha lugha zote za Kibantu.

Tabia za Kibantu na historia ya lugha

Lugha za Kibantu zina tabia mbalimbali za pamoja. Kati ya tabia hizo kuna viambishi awali na ngeli za nomino.

Kutokana na sifa hizo wataalamu wamekadiria kwamba asili ya lugha za Kibantu ilikuwa katika maeneo ya Kamerun ya Kusini; kutoka huko wasemaji asilia wa Kibantu walihamia katika milenia ya pili KK Kongo hadi Zambia. Waliendelea kuhamahama na kupanuka hadi kufika maeneo yote walipo sasa. Sehemu kubwa ya maeneo ya wasemaji wa lugha za Kibantu zilikaliwa awali na wasemaji wa lugha za Khoikhoi. Wataalamu wamekisia kwamba Wabantu walifaulu kunea kutokana na maarifa yao ya kilimo na hasa matumizi ya chuma katika zana za kilimo na pia silaha.

Kati ya lugha za Kibantu zinazotumika zaidi kuna Kiswahili na Kilingala. Lugha zenye wasemaji wengi kama lugha ya kwanza ni Kizulu na Kishona.

Lugha za Kibantu zenye wasemaji wengi

(Idadi ya wasemaji ni makadirio tu; bado ina tofauti kati ya makala na makala)