Papa Paulo I
Mandhari
Papa Paulo I alikuwa Papa kuanzia mwezi Aprili au tarehe 29 Mei 757 hadi kifo chake tarehe 28 Juni 767[1]. Alitokea Roma, Lazio, Italia[2] katika familia Orsini[3] [4].
Alimfuata Papa Stefano II ambaye alikuwa kaka yake, akafuatwa na Papa Stefano III.
Kabla ya kuteuliwa Papa alikuwa shemasi na kutumwa na kaka yake kupatana na Walombardi waliotawala sehemu kubwa ya Italia. Alichaguliwa ili kuendeleza sera hiyo, naye alijitahidi kutetea haki za Kanisa kwa msaada wa mfalme wa Wafaranki, Pipino Mfupi, ingawa kwa kufanya hivyo alimchukiza kaisari wa Dola la Roma Mashariki[5].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa kwenye tarehe ya kifo chake[6].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Mapapa
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ McClintock, John; Strong, James (Aprili 15, 1882). Cyclopaedia of Biblical, Theological, and Ecclesiastical Literature. Juz. la VII. Harper. uk. 831 – kutoka Internet Archive.
Pope Paul I.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ George L. Williams, Papal Genealogy (London 2004).
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/89093
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Paulo I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |