[go: nahoru, domu]

Nenda kwa yaliyomo

Saturninus bin Saturninus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Saturninus bin Saturninus ni jina la mmojawapo katika kundi la Wakristo 49 ambao mwaka 304, wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian, walihukumiwa kwa kuadhimisha Siku ya Bwana huko Abitinae[1][2][3], mji wa Afrika Kaskazini (leo Tunisia).

Tarehe 24 Februari mwaka 303, Diokletian alikuwa ametangaza hati yake ya kwanza dhidi ya Wakristo, akiagiza uteketezaji wa Biblia na maabadi ya Kikristo katika Dola la Roma lote, pamoja na kukataza Wakristo wasikutane kwa ajili ya ibada.[4]

Ingawa Fundanus, askofu wa Abitinae, alikubali kukabidhi maandiko matakatifu ya Kanisa kwa serikali, baadhi ya waamini waliendelea kukutana kwa siri chini ya padri Saturninus, baba wa Saturninus. Basi, walikamatwa na kupelekwa na mahakimu wa huko hadi Karthago, makao makuu ya mkoa, kwa ajili ya hukumu.[5]

Tarehe 12 Februari gavana Anullinus alisikiliza kesi. Mmoja wa watuhumiwa, Dativus, alikuwa mjumbe wa senati. Ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhojiwa, kuteswa na hatimaye kufa.[6][7]

Saturninus alifuata na kushika msimamo katika kuteswa. Wote walifanya vilevile, wanaume kwa wanawake wakiwemo watoto wake 4.

Kati ya majibu waliyotoa hao wafiadini, moja limetajwa mara nyingi: Emeritus, aliyekuwa mwenyeji wa wenzake, alipoulizwa kwa nini aliwakaribishwa kwa ibada kinyume cha sheria, alijibu: "Sine dominico non possumus" ("Hatuwezi kuisi bila ya Bwana").

Tangu kale wafiadini hao wote wanaheshimiwa kama watakatifu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 12 Februari. [8]

Orodha ya wafiadini wa Abitina

[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Jean-Yves Congar, Encyclopedia of Christian Theology (Taylor & Francis 2004 ISBN 978-0-20331901-7). vol. 1, p. 499
  2. Annuario Pontificio 2013 (Libreria Editrice Vaticana 2013 ISBN 978-88-209-9070-1), p. 822
  3. Sancti Aureli Augustini Scripta contra Donatistas, pars I, p. 359
  4. Bleckmann, Bruno. "Diocletianus." In Brill's New Pauly, Volume 4, edited by Hubert Cancik and Helmut Schneider, 429–38. Leiden: Brill, 2002. ISBN 90-04-12259-1
  5. Santi Martiri di Abitina
  6. Dictionary of Christian Biography and Literature to the End of the Sixth Century A.D., with an Account of the Principal Sects and Heresies
  7. Dativo e i martiri di Abitina Archived Septemba 1, 2008, at the Wayback Machine
  8. Under that date the Roman Martyrology records the names of all forty-nine: Martyrologium Romanum (Libreria Editrice Vaticana, 2001 ISBN 88-209-7210-7)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]